
“Kwa niaba ya viongozi wenzangu wa SNC kwa muhula wa 2022 – 2025 nipende kutoa shukrani za dhati kwa Washiriki na Watumishi wote wa SNC kwa ushirikiano, bidii na moyo mkuu uliowezesha kufanyika kwa kazi ya utume katika kipindi hiki. Mungu wetu mwenye pendo aendelee kuwabarikia na kuwatia nguvu.”
–Pr. Onesmo M. Daniel.

“Napenda kuchukua fursa hii adhimu kumshukuru Mungu wetu mwenye rehema kwa kutuwezesha kukutana tena katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa South Nyanza Conference. Neema yake ya ajabu iliyotuwezesha kufika hapa ikaendelee kutuongoza kuutekeleza utume wetu katika kipindi hiki cha kufungwa kwa historia ya ulimwengu”
–Pr. Beatus G. Mlozi

“Sisi watu wa SNC tuna kila sababu ya kuutangaza ukweli ule wa Zaburi 124:1 maana kwa kweli Bwana amekua pamoja nasi. Tunapokutana tena katika mkutano mkuu huu wa 9 tunatazamia baraka za Bwana ziendelee kuandamana nasi katika muhula huu mpya unaoenda kuanza”
–Eld. Mwita J. Machage
9
MKUTANO MKUU WA TISA WA SOUTH NYANZA CONFERENCE
Mkutano Mkuu wa Tisa 2025 wa Conferensi ya South Nyanza Unafanyika ana kwa ana katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Kirumba Siku ya Jumatatu, Septemba 29, 2025. Unahudhuriwa na wajumbe 378 wakiwa ni wawakilishi wa makundi mbalimbali ndani ya South Nyanza Conference.
297
Wajumbe Wawakilishi kutoka Makanisa ya South Nyanza Conference.
378
Jumla ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa SNC.
81
Wajumbe Wawakilishi wa Makundi Mengine.